Mawkib hii, huduma mbalimbali za kijamii zinatolewa kwa Wananchi wa maeneo hayo, sambamba na kusambaza ujumbe wa Aba Abdillah Al-Hussein (as) wa kuhuisha maadili na misingi ya Kiislamu; kuhimiza kusema ukweli na haki, pamoja na kueneza uadilifu kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Binadamu.

2 Julai 2025 - 23:02

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA
Katika muktadha wa Kuadhimisha kumbukumbu ya Shahada ya Aba Abdillah Al-Hussein (as), Husseiniyyah ya Hazrat Qamar Bani Hashim (as), iliyopo Ulongoni B, Dar es Salaam, Tanzania, imeweka Mawkib ya Aba Abdillah Al-Hussein (as) ikiendeshwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za Kijamii kama vile kugawa maji safi ya kunywa, Chocolate, Chakula na vipeperushi vyenye Ujumbe na Mafunzo Muhimu ya Kiislamu kutoka Imam Hussein (as), Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saww).

Uanzishwaji wa Mawkib ya Aba Abdillah Al-Hussein(as) - Ulongoni B, Dar es Salaam, Tanzania ikiendeshwa na Husseiniyyah ya Hazrat Qamar Bani Hashim(as)

Mawkib hii pamoja na Majlisi mbalimbali za Maombolezo ya Muharram, zinaendeshwa na Husseiniyyah ya Hazrat Qamar Bani Hashim (as) chini ya uongozi na usimamizi wa Mudir wake, Samahat Sheikh, Al-Muhtaram Salum Bendera.

Mwamko umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na juhudi madhubuti zinafanyika kwa lengo la kumtambulisha Imam Hussein (as) pamoja na Ahlul-Bayt (as) kwa ujumla kwa wananchi wa Tanzania.

Kama tulivyodokeza hapo juu, kupitia Mawkib hii, huduma mbalimbali za kijamii zinatolewa kwa Wananchi wa maeneo hayo, sambamba na kusambaza ujumbe wa Aba Abdillah Al-Hussein (as) wa kuhuisha maadili na misingi ya Kiislamu; kuhimiza kusema ukweli na haki, pamoja na kueneza uadilifu kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Binadamu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha